Kampuni ya Vinywaji baridi nchini ya Coca cola imeahidi kuendelea kusaidia Mashindano ya Umiseta ambayo hufanyika kila mwaka yakijumuisha timu za secondary kwa nchi nzima na kuahidi kushirikiana na Serikali katika kutatua matatizo  yanayo ikumba sekta ya michezo.

Hayo yamesemwa naAfisa Masoko wa kampuni hiyo Bi,Mariam Sezinga alipokua akiongea na Waandishi wa habari mapema hii leo jijini Dar es salaam,Bi,Mariamu aliongeza kuwa kupitia kampuni ya Coca cola wataendelea  kusaidia mashindano hayo ili kuweza kuyaboresha zaidi.

Aidha Bi,Mariam alisema  wapo tayari kuendelea kudhamini Mashindano hayo  ili kuweza kuinua vipaji vya Vijana wanaochipukia katika tasnia hiyo ya mpira wa miguu nchini,na kwamba kila kitu huandaliwa mapema na baadae kuweza kufaidi matunda.

Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo Tanzania Bw,Mohamed Kiganja aliishukuru kampuni  hiyo na  kuwataka kuendelea kushirikiana na Serikali katika kuendeleza mpira hapa nchini kwani hilo siyo jukumu la serikali peke yake bali ni jukumu la wote kuhakikisha mpira wa miguu unasonga mbele.

Kwa upande wake Mwalimu wa Michezo kutoka kibasila sekondari Bw,Abel Tweve aliyekua kaongozana na viongozi hao alitoa wito kwa wazazi na walezi kuwaruhusu watoto wao kushiriki katika Michezo kwani  michezo ni ajira na ina inua kipato cha familia na nchi kwa ujumla

Video: 'Gwajima Tunamtafuta sana' - Kamanda Sirro
NAPE NNAUYE AZINDUA RADIO YA KIJAMII JIJINI DAR ES SALAAM