Kocha Mkuu wa Klabu ya Chelsea, Antonio Conte amesema kuwa anafuraha kubwa kubaki na Klabu hiyo licha ya uvumi kwamba uhusiano wake na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abrahamovic umedorora.

Conte mwenye umri wa miaka 48 aliiongoza Blues kushinda taji la ligi kuu Uingereza msimu uliopita na sasa timu hiyo iko katika nafasi ya tatu, wakiwa wameachwa pointi 15 na vinara wa ligi hiyo Manchester City.

Aidha, mmiliki wa timu hiyo, Abrahamovic alikasirishwa na matamshi ya kocha huyo kwamba hakuhusishwa katika kuchagua wachezaji watakaojiunga na klabu hiyo msimu huu.

”Jukumu langu ni kujaribu kutoa matokeo bora ,kujaribu kuwaimarisha wachezaji wangu katika klabu hii ili iweze kuendelea kutoa mataji,”amesema Conte

 

Manara aihofia Maji Maji
Video: Lowassa atoboa siri, Wamekwisha