Wajumbe katika mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mazingira wa COP27 wamefikia makubaliano ya kihistoria ambayo yataanzisha mfuko maalum wa kuzifidia nchi maskini ambazo zinaathiriwa zaidi na mabadiliko ya tabianchi.

Makubaliano ya kuundwa kwa mfuko wa kuzifidia nchi maskini zinazoathiriwa na uchafuzi wa gesi ya kaboni unaosababishwa na nchi tajiri, yamefikiwa jumapili hii katika kikao cha mashauriano kwenye mkutano huo unaofanyika kwenye mji wa mapumziko wa Sharm el-Sheikh nchini Misri.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri, Sameh Shoukry ambaye pia ni Rais wa COP27, alipendekeza kuanzishwa kwa mfuko huo Jumamosi mchana na kufikiwa na pande husika siku hiyo.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri na Rais wa COP27, Sameh Shoukry

Hata hivyo makubaliano makubwa bado hayajafikiwa kwa sababu ya mvutano uliopo kuhusu juhudi za kupunguza matumizi ya gesi ya kaboni inayochafua mazingira.

Maamuzi muhimu juu ya kuachana na nishati zote za mafuta na makaa ya mawe na kuweka kikomo cha ongezeko la joto kwa nyuzi joto 1.5 katika kipimo cha Celsius, kilichokubaliwa katika katika mkutano wa COP26 uliofanyika mwaka 2021 huko Glasgow, bado hayajafikiwa.

Mfuko huo uliopewa jina “hasara na uharibifu” umekuwa ajenda rasmi kwa mara ya kwanza katika mkutano wa kilele wa COP27, baada ya shinikizo kuongezeka kutoka katika nchi zinazoendelea.

Wajumbe wamepongeza kuanzishwa kwa mfuko huo kufuatia wiki mbili za mazungumzo yenye utata kuhusu matakwa ya mataifa yanayoendelea kwa mataifa tajiri ambayo ni wachafuzi wa mazingira, kuwafidia kutokana na uharibu na majanga yanayosababishwa na hali mbaya ya hewa.

WajumbE wa Mkutano wa COP27

Mfuko huo unahusisha athari nyingi zitokanazo na hali ya hewa, kuanzia madaraja na nyumba zilizosombwa na mafuriko, hadi kitisho cha kutoweka kwa tamaduni na visiwa vyote, hadi kuongezeka kwa kiwango cha bahari.

Mwaka huu majanga yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi kuanzia mafuriko makubwa nchini Pakistan hadi ukame mbaya unaotishia baa la njaa nchini Somalia, yalitiliwa mkazo zaidi katika nchi zilizokumbwa na maafa, ambazo tayari zilikuwa zikipambana na mfumuko wa bei pamoja na madeni yanayoongezeka.

Trump arejea Twitter
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 20, 2022Â