Kila jambo huja na maajabu yake! Katika hali ya kushangaza, mwanaume mmoja anashikiliwa na polisi nchini Urusi kwa kosa la kuwafyatulia risasi na kuwaua watu watano kwa madai kuwa waligoma kupunguza sauti zao wakiwa karibu na nyumba yake, huku kukiwa na marufuku ya kutembea nchini humo.

Tukio hilo linadaiwa kutokea katiak Kijiji cha Yelatma katika mkoa wa Ryazan ulioko Magharibi mwa nchi hiyo. Eneo hilo liko katika marufuku ya kutoka nyumbani, wakati nchi hiyo ikiwa inapambana na kusambaa kwa virusi vipya vya corona (covid-19).

Kamati ya Upelelezi ya Urusi imeliambia Shirika la Habari la TASS kuwa Mwanaume huyo alianza kubishana na jirani zake akiwa amesimama kwenye kibaraza (balcony) ya nyumba aliyokuwa anaishi, wakati wao wakiendelea kuongea kwa sauti ya juu.

Ilieleza kuwa waliouawa ni pamoja na wanaume wanne na mwanamke mmoja. “Aliwataka vijana hao wanne na msichana mmoja ambao walikuwa wanaongea kwa sauti ya juu karibu na nyumba yake kuacha mara moja, lakini walipoendelea aliwafyatulia risasi na kuwaua wote,” ilieleza.

“Maafisa wa Polisi walifika katika eneo la tukio na kumkamata wanaume huyo mwenye umri wa miaka 32,” taarifa ya Idara ya Wizara ya Mambo ya Ndani ilikaririwa na TASS, Jumapili, Aprili 5, 2020.

 

Nchi mbili pekee hazijaathirika na Corona Afrika
Kumbukizi miaka 48 ya kifo cha Karume aliyekatishwa maisha yake

Comments

comments