Klabu ya Azam FC, leo hii Machi 18, 2020, imevunja rasmi kambi yake na kuwaruhusu wachezaji wote kurudi makwao.

Hii ni kufuatia tamko la serikali hapo jana, Machi 17, 2020, kupitia Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

Katika tamko lake, Mheshimiwa Majaliwa alitangaza kusimamisha kwa mwezi mmoja shughuli kadhaa zinazosababisha msongamano wa watu, ikiwemo mechi za mpira wa miguu, kutokana na mlipuko wa maradhi ya virusi vya corona, ambavyo vimeingia nchini.

Kutokana na hilo, kambi zote, kuanzia ile ya vijana chini ya miaka 17, vijana chini ya miaka 20 na timu ya wakubwa, zimevunjwa mara moja.

Kambi hizo zitarejea tena Aprili 17, 2020, ambao ni mwezi mmoja kamili kama alivyoagiza Waziri Mkuu.

Azam FC inaungana na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Shirika la Afya Duniani, WHO, katika kutoa wito kwa wananchi kufuata maelekezo ya kitaalamu ili kujilinda na maambukizi ya maradhi haya hatari.

Video: Korona yavuruga, Lissu ataja vikwazo kurejea
CORONA: Ligi Tanzania kuchezwa bila mashabiki