Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limetangaza maamuzi magumu kuhusiana na michuano ya ligi ya mabingwa barani humo (UEFA Champions League) na kombe la shirikisho (UEFA Europa League) wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona.

UEFA wametangaza kuahirisha michezo ya michuano hiyo kwa muda usiojulikana kutokana na mlipuko wa virusi vya Corona kuendelea kushika kasi, barani Ulaya na kwingineko duniani.

Licha ya michuano hiyo kuwa imesimamishwa kwa muda usiojulikana, lakini inaripotiwa inaweza kuendelea Julai au Agosti 2020, hii pia ni kupisha Ligi za ndani ziweze kumalizika na kuangalia maambukizi ya Corona kama yatakuwa yamepungua.

Wakati huo huo nahodha wa Aston Villa Jack Grealish ameomba radhi baada ya kuvunja agizo la Serikali la kujifungia ndani wakati huu wa mlipuko wa virusi vya Corona.

Grealish, amesema rafiki yake ndiye amemshawishi kufanya kosa hilo. Amesema kila mtu kujifungia ndani ni wakati mgumu kwa sasa, na alipata simu kutoka kwa rafiki yake akitaka akamuone kwake, na kwa ujinga, alikubali kufanya hivyo.

Amesisitiza kuwa hataki mtu yeyote afanye kosa kama hilo. Licha ya kuomba radhi kwa kukaidi agizo la serikali klabu yake imempiga faini ya Pauni 150,000 ambayo itatolewa kama msaada katika Hospitali ya kijamii ya Chuo Kikuu cha Birmingham.

Kampuni 10 zatangaza nafasi za ajira hapa
Mexime awashangaa mashabiki wa Simba, Young Africans