Diamond Platinumz ameonesha kuguswa na changamoto ya kiuchumi inayowakabili Watanzania wengi kutokana na athari za mlipuko wa virusi vipya vya corona (covid-19), na kutangaza kutoa msaada wa kodi ya nyumba ya miezi mitatu kwa familia 500.

Bosi huyo wa lebo ya muziki ya WCB na mmoja wa wamiliki wa Wasafi FM/TV, ameeleza nia yake kupitia mtandao wa Istagram akiweka picha yenye maandishi ‘Shida yako ni Shida Yangu.’

Najua katika kipindi hiki cha Corona, mambo mengi hayajakaa sawa, hususan upande wa biashara….nyingi zimeshuka na kupelekea hali ya kifedha kuyumba na mambo kuwa kidogo Magumu kwa wengi wetu…ijapokuwa na mimi ni Miongoni mwa walio ndani ya janga hili, lakini nimeona walau kwa kidogo changu nilicho nacho, nitoe kusaidia kulipia kodi za Nyumba kwa miezi Mitatu mitatu kwa familia 500, walau kusaidiana Katika kipindi hiki kigumu cha kupambana na Virusi hivi vya Corona…Licha ya kuwa Tiafa moja lakini siku zote mmekuwa Familia yangu kupitia Muziki wangu, hivyo naamini Shida yenu ni yangu, na Tabasamu lenu ni Langu pia….Jumatatu nitaweka rasmi Utaratibu wote wa namna gani Familia Hizi Miatano zinaweza kupata kodi hizo ya Nyumba….🙏🏼

#HiliNaloLitapita #ShidaYakoNiYangu #PamojaTutaishindaCorona

Kenyatta: Wakenya hawatatumika kama wanyama kujaribu dawa ya corona
JPM asamehe wafungwa 3,973, atoa ujumbe maadhimisho ya Muungano

Comments

comments