Virusi vipya vya corona (Covid-19) vimesababisha vifo vingi nchini Italia zaidi ya nchi yoyote duniani baada ya kupanda hadi vifo 427 kwa siku moja.

Hali hiyo imesababisha kuwa na jumla ya watu 3,405 waliopoteza maisha kutokana na virusi vya corona nchini humo, idadi ambayo inazidi idadi ya China ambapo panaaminika kuwa virusi hivyo vilianzia mwaka jana.

China ambayo imewekeza kwa nguvu katika mapambano dhidi ya kusambaa kwa virusi hivyo imeripoti idadi ya vifo 3,245 hadi Machi 19, 2020.

Kutokana na hatari ya virusi hivyo, Serikali ya Italia imeongeza muda wa watu kukaa majumbani kutoka Machi 25, 2020 hadi watakapotangaziwa tena.

Ingawa kumekuwa na juhudi kubwa ya kukabilia na ugonjwa huu duniani kote, idadi ya visa imezidi kuongezeka. Hadi sasa kuna visa 220,000 na vifo zaidi ya 9,000 vilivyoripotiwa duniani kote.

Membe aibuka tena na uchaguzi 2020, aeleza alichosema alipohojiwa
CORONA: Wageni kutoingia Bungeni Dodoma