Wizara ya Afya nchini Uhispania leo imetangaza kuwa karibu watu 950 wamefariki ndani ya saa 24 kutokana na Homa Kali ya Mapafu Covid-19 na kufanya idadi ya waliopoteza maisha kutokana na ugonjwa huo kufikia 10,300.

Idadi hiyo ni kubwa zaidi kutokea nchini humo kwa siku moja ambapo Uhispania ni moja kati ya nchi zinazotajwa kuathirika vibaya na Corona.

Aidha Uhispania ina maambukizi 112,065 ikizifuata Marekani yenye maambukizi 245,175 na Italia yenye maambukizi 115,242, huku ikishika namba mbili duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya vifo ikitanguliwa na Italia yenye jumla ya vifo 13,900.

Wanaotumia jina la Simba SC waonywa
CORONA: Hatma ya EPL bado kitendawili

Comments

comments