Idadi ya vifo kutokana na virusi vya corona imepanda jana na kupindukia 20,000 barani Ulaya, huku Italia na Uhispania kila moja ikiripoti vifo vya zaidi ya watu 800 katika siku moja.

Imeelezwa kuwa takribani theluthi moja ya idadi ya watu duniani wamefungiwa majumbani wakati virusi hivyo vikiendelea kuvuruga kila muhimili wa jamii kwa kusababisha vifo na ukosefu wa ajira.

Kote ulimwenguni, idadi ya vifo imepindukia 30,000 na maafisa katika baadhi ya nchi wanasema hali itaendelea kuwa mbaya katika siku zijazo.

katika mji wa Wuhan nchini China ambao virusi hivyo vilianzia, maafisa wameanza kuchukua hatua za kurejesha hali ya kawaida, kwa kufungua kwa sehemu mji huo baada ya karibu miezi miwili ya kufunga kabisa mji huo wenye idadi ya watu milioni 11.

Ulega: Minada ya Ng’ombe na Samaki isifungwe kwa Corona
Kenya: idadi ya waliothibitika kuwa na Corona yaongezeka