Visa vya maambukizi ya virusi vya Covid -19 nchini Kenya vimeendelea kuongezeka  na kufikia 122 baada ya watu 12 kugundulika wameathirika leo huku mtoto wa miaka 6 akipoteza maisha.

Waziri wa Afya nchini humo, Dkt. Mercy Mwangangi leo Aprili 3 ametangaza visa hivyo na kubainisha kuwa wagonjwa walioongezeka 11 ni raia wa kenya na mmoja ni msomali

Dkt. Mwangangi amesema kuwa mtoto huyo aliyefariki ni wakiume, na alikuwa akipatiwa matibabu hospitali ya taifa Kenyatta.

Aidha amebainisha kuwa hadi kufika siku ya leo, Ijumaa, watu 1, 433 waliopo karantini wamepimwa corona na wengine 617 wanatarajiwa kupimwa pia.

Video: Corona yamfikisha Masanja Polisi
UEFA yatahadharisha wanaomaliza ligi mapema

Comments

comments