Marekani imeripoti vifo 1,736 vilivyotokea jana, Jumanne, idadi kubwa zaidi kurekodiwa ndani ya siku moja, ambapo asilimia kubwa ya vifo hivyo vimetokea Jijini New York.

Jumla ya waliofariki kutokana na Virusi vya Corona nchi humo imefikia 12,854. Maambukizi yaliyorekodiwa nchini humo mpaka sasa ni 400,412, idadi ambayo ni kubwa zaidi duniani.

Wataalamu wa Afya kutoka Ikulu ya Marekani ‘White House’ wametabiri kuongezeka zaidi kwa Vifo vya wagonjwa wa Covid-19, na kwamba kadri ya watu 100,000 hadi 240,000 wanaweza kupoteza maisha kutokana ugonjwa huo hata kama maagizo ya kukaa nyumbani yakifuatwa.

Rais wa Marekani Donald Trump ametishia kusitisha kutoa fedha kwa Shirika la Afya Duniani (WHO) huku akilishutumu Shirika hilo kwa kuipendelea China na kushindwa kudhibiti mlipuko huo ambao umegharimu maisha ya watu 82,080 duniani kote.

Aidha wataalamu wa afya wamesema hali inaweza kuwa mbaya zaidi wiki hii ambapo Miji ya New York, New Jersey, Connecticut na Detroit imetajwa kuwa katika hatari zaidi.

Mgonjwa mpya wa Corona Kenya alitembelea Tanzania
Luc Eymael athibitisha hitaji la maproo wanne