Mshambuliaji wa mabingwa wa soka nchini Italia Juveentus FC Cristiano Ronaldo, ameitwa “mzururaji” na kuamuriwa aondoke katika mji wa Madeira nchini Ureno.

Ombi hilo kwa Ronaldo limetolewa na mwanasiasa Rafael Macedo, baada ya picha kuibuka zikimuonyesha nahodha huyo wa kikosi cha timu ya taifa ya Ureno akitembea mitaani na familia yake wakati huu wa janga la ugonjwa wa Corona.

Kwa mujibu wa tovuti ya The Sun ya Uingereza, mwanasiasa huyo, alimshambulia vikali Ronaldo katika mtandao wa kijamii wa Facebook baada ya kuona picha zake akiwa anatembea na mpenzi wake Georgina Rodriguez na watoto wao katika mji huo ambao ndipo mwanasoka huyo alipozaliwa.

Mwanasiasa huyo aliandika “Namtaka mnyama huyo aliyekuja kutoka Italia kukaa nyumbani. Niondoleeni mzururaji huyo katika mji wa Madeira.”

Lakini katika andiko lingine katika Facebook, Macedo alisema akaunti yake ilidukuliwa hawezi kutoa kauli mbaya kama hiyo dhidi ya CR7 wao.

Hii sio mara ya kwanza jambo kama hili kutokea, na tayari ameshabadilisha password zake. Aidha katika hatua nyingine alichukua fursa ya kumuomba radhi kila mtu hasa Ronaldo na familia yake ambao amesema anawathamini sana, kwa kile kilichotokea.

Mexime awashangaa mashabiki wa Simba, Young Africans
Madaktari waomba vifaa vya kujikinga na Corona