Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imethibitisha kuwepo kwa mgonjwa mpya mmoja mwenye maambukizi ya virusi vya Corona (COVID-19), Mgojwa huyo ni mwanaume mwenye umri wa miaka 51 raia wa Tanzania mkazi wa Dar Es Salaam na kufanya  jumla ya wagonjwa kuwa 25.

Mapema leo ubalozi wa China nchini Tanzania umeipatia Serikali msaada wa vifaa kinga kwaajili ya kuendelea kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Covid 19 (Corona), na kuahidi kuendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kukabiliana na ugonjwa huo, hadi hapo utakapomalizika.

Akipokea vifaa hivyo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amesema msaada huo utaenda kwa watumishi wa afya kote nchini kwani serikali imetoa kipaumbele cha kwanza kwao ili kuweza kuwakinga na maambukizi ya Covid-19.

“kwa niaba ya serikali tunaishukuru sana Serikali ya China kwa mchango huu, na niendelee kuwathibitishia wale wote mnaoisaidia Serikali ya Tanzania,msaada huu tutaupeleka kwa watumishi wa afya,kipaumbele ni kuwakinga watumishi wa afya wasipate maambukizi” Amesema Ummy

Msaada huo uliotolewa na ubalozi wa China nchini Tanzania ni pamoja na mavazi (PPE) 1,000 ya kujikinga wakati wa kuhudumia watu waliothibitika kuwa na ugonjwa wa corona, Barakoa (Mask) 100,000 pamoja na Vipima joto vya mkono(thermal scanner) 150.

Kwa upande wake balozi wa China nchini Tanzania, Wang Ke amesema nchi yake na Tanzania ni marafiki kwa muda mrefu na ugonjwa huo ulipoikumba nchi yao kwa mara ya kwanza, Tanzania ilikuwa mstari wa mbele kuwaunga mkono katika mapamabano dhidi ya ugonjwa huo, hivyo na wenyewe wamejitoa kuisaidia kukabiliana nao.

Katika mwendelezo wa kuisadia vifaa kinga Serikali ya Tanzania, kwa mara nyingine tena inatarajia kupokea msaada wa vifaa tiba vya kusaidiawagonjwa kupumua (Ventilator) 500 kutoka kwa mfanyabiashara raia wa China Jack Ma.

Pierpaolo Marino atabiri EPL kufutwa
Ali Kiba afunguka uhusiano wake na Hamisa, ‘nampenda’