Serikali nchini Kenya imethibitisha kuwepo kwa mgojwa wa kwanza wa virusi vya Corona mapema leo Machi 13, 2020.

Mgonjwa huyo ni mwanamke waliyesafiri hivi karibuni kutoka Marekani akipitia London, hali yake kwa sasa inaendelea vizuri ila hataruhusiwa kutoka mpaka vipimo vitakapodhibitisha hana maambukizi.

Serikali  ya nchi hiyo imewataka wananchi kuwa watulivu wakati ikichukua hatua madhubuti na imesitisha ndugu kutembelea magereza kwa siku 30 zijazo.

Barani Afrika nchi nyingine ambazo Virusi hivyo vimeripotiwa ni Misri, Nigeria, DRC, Morocco, Burkina Faso, Togo, Algeria, Tunisia, Afrika Kusini, Cameroon, Senegal na Ivory Coast.

Nchi za Ghana na Gabon zimeripoti kupata maambukizi ya Virusi vya Corona kwa mara ya kwanza.

Taarifa ya Serikali ya Gabon imeeleza kuwa aliyeambukizwa ni Raia wa miaka 27 aliyerudi nchini humo akitokea Ufaransa.

Wizara ya Afya ya Ghana imeripoti maambukizi ya watu wawili ambao wametokea Uturuki na Norway. Wawili hao tayari wapo karantini na wanaendelea vizuri.

Mnyika na wenzake wachomoka Segerea, Mbowe abaki pekeyake
Corona: Kocha wa Arsenal aambukizwa, Beki wa Man City atengwa