Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amelazwa Hospitali ya Mtakatifu Thomas jijini London katika chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) baada ya afya yake kuzorota kutokana na virusi vya corona.

Ofisi yake imesema Johnson alikuwa akipokea uangalizi wa karibu sana lakini alipelekwa katika chumba hicho kutokana na ushauri wa madaktari wake.

Waziri huyo amemtaka waziri wa maswala ya kigeni Dominic Raab kumsaidia kazi zake za kiofisi kwa muda huu anaoumwa pale atakapoweza.

Tokea alipolazwa siku ya Jumapili jioni, viongozi mbalimbali duniani akiwemo rais Donald Trump na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wamemtumia salamu za pole.

Kumbukizi miaka 48 ya kifo cha Karume aliyekatishwa maisha yake
Rais FIGC akataa kufuta msimu wa Serie A

Comments

comments