Korea Kusini imeripoti ongezeko la mara nane la maambukizi ya virusi vya corona katika kipindi cha siku nne na idadi ya maambukizi imefika watu 433.

Maambukizi mengi yanatajwa kutokea katika hospitali moja na kanisa la mji wa Daegu, huku wahudumu wa afya wakiendelea kuwafanyia uchunguzi waumini wapatao 9,000.

Iran pia imeripoti leo kifo cha mtu mmoja na visa vyengine 10 vya maambukizi, na kuifanya idadi ya vifo kufika watu watano na walioambukizwa virusi hivyo kufika watu 28.

Na nchini Japan kumeripotiwa pia ongezeko la visa vya maambukizi ya virusi hivyo vya corona, jumla imefika visa 755, huku zaidi ya visa 630 vikiwa ni katika meli ya Diamond Princess.

Togo wafungua pazia uchaguzi wa marais Afrika 2020
Jacqueline Mengi alia kufukuzwa kwenye kaburi la mumewe

Comments

comments