Afisa Mtendaji Mkuu na Msimamizi wa Hakimiliki Tanzania Doreen Anthony Sinare amepokea mapendekezo ya taarifa ya Kamati ya Kuratibu Usambazaji wa kazi za Filamu kwa vyombo vya Usafirishaji kama mabasi kutoka kwa kamati iliyoundwa na Shirikisho la Filamu Tanzania.


Kamati hiyo imetoa mapendekezo ya utaratibu wakusambaza Filamu zitakazo kuwa zinaoneshwa katika vyombo vya usafirishaji kwa lengo la kuhakikisha filamu hizo zimekidhi vigezo vya utaratibu wa usambazaji kwa lengo la kulinda hakimiliki na wamiliki kuweza kufaidika na ugawaji wa mirabaha.


Akizungumza katika kikao hicho Afisa Mtendaji Mkuu huyo amesisitiza Kamati hiyo kuharakisha upatikanaji wa kazi hizo kwani tayari ameshafanya mazungumzo na uongozi wa DART na wako tayari kuingia makubaliano ili mabasi yao yaweze kuonesha kazi hizo.

Naye Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania Eliah Mjata ameishukuru COSOTA kwa namna wanavyotoa ushirikiano na kuahidi kukamilisha jambo hilo kwa haraka ndani ya mwezi huu.

Mazungumzo ya kuunda serikali yafikia pazuri Ujerumani
Simulizi: Penzi la Mke wa jirani yangu lilivyotaka kumaliza uanaume wangu