Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Amos Nungu leo ameongea na vyombo vya habari kuufahamisha umma kuwa Tume imejiridhisha na barua iliyokuwa inasambaa mitandaoni ni barua halali iliyotolewa kwa Taasisi ya Twaweza ili kupata ufafanuzi wa utafiti wao.

Mkurugenzi huyo amesema Tume imesikitishwa kuona mawasiliano halali ya kiofisi yanapelekwa mtandaoni hata kabla ya kupata majibu rasmi kwa mtu aliyepelekewa barua hiyo.

Julai 5, 2018 Taasisi ya Twaweza ilitoa matokeo ya utafiti ambao ulizungumzia hali ya siasa ambapo imesema umaarufu wa Rais John Pombe Magufuli umeshuka kwa 55% kwa mwaka huu huku 2016 ulikuwa ni 96%.

Aidha kumekuwa na barua iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii iliyoandikwa na COSTECH iliyoitaka taasisi ya Taweza kuchukuliwa hatua mara baada ya kutangaza utafiti wake bila kupata kibali maalumu toka Taasisi ya COSTECH.

Kwa upande wa Twaweza, Meneja Utetezi Anastazia Rugaba alikiri kupokea barua hiyo toka (COSTECH) na kusema watajadili swala hilo mara baada ya barua hiyo kupitiwa.

Luis Nani arudi nyumbani
Gari la wagonjwa lanaswa likisafirisha mirungi kwa ving’ora