Hatimaye msanii wa muziki wa Hip Hop Tanzania Ibrahim A. Mandingo maarufu Country Wizzy ameachana rasmi na ‘Konde Music World wide’. Label ya muziki inayomilikiwa na msanii Harmonize baada ya kumaliza mkataba wake.

Baada ya taarifa za awali zilizotolewa kupita ukurasa maalum wa Label hiyo, CEO wa Label hiyo msanii Harmonize naye kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram ameandika maneno machache ya kumshukuru na kumpongeza kwa kushirikiana naye katika kazi kwa kipindi cha miaka miwili mfululizo.

“Asante kwa kuliwakilisha chama kubwa kwa kipindi cha miaka miwili, nakupenda ndugu yangu na ninakutakia kila la heri, nenda kanifanye nijivunie wewe, nenda kang’ae rasta” aliandika Harmonize aakiambatanisha na picha ya Country Boy.

Licha ya Harmonize kuiweka taarifa hiyo hadharani kwa kumuaga rasmi Country Boy leo januari 9, 2022, zipo tetesi za msanii huyo kujitoa Konde Music ambazo zilianza kuenea kwa kasi kote mitandao mapema jioni ya Januari 7, 2022.

Hata hivyo wametajwa wasanii wengine walio chini ya Label hiyo Killy na Cheed kuwa nao wako mbioni kujiengua japo tatizo ni kwamba mkataba waliosaini na ‘Konde Music World Wide’ unawahitaji kulipia gharama za kuvunja mkataba kwa mujibu wa makubalino yao.

Saido aiweka roho juu Young Africans
Akamatwa na jino la Tembo darini