Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko – CPB, imetekeleza kwa vitendo juhudi za Rais Samia Suluhu Hassani katika kukuza sekta ya Kilimo nchini, kwa kuwahudumia wananchi na kuwapa ahueni kwa kuwauzuia bidhaa zao kwa bei nafuu na zenye ubora.

Aidha CPB imelenga kukuza Uchumi wa Nchi na Mwananchi mmoja moja kwa kuuza bidhaa zao nje ya nchi na ndani ya nchi lakini katika ubora unaozingatia Afya kwa maana ya kuhakikisha virutubisho vyote vilivyomo katika Nafaka vinakuepo katika bidhaa zao.

Akizungumza hivi karibuni, Meneja wa Nyanda za Juu za Kusini wa CPB Dkt Samweli Jasper alisema Bodi hiyo ipo kwa ajili ya Wananchi kwa kuwapa bidhaa iliyo bora lakini kwa kuwauzia kwa bei nafuu kwani hilo ndio lengo la Serikali ya Rais Samia.

Meneja wa CPB Nyanda za Juu Kusini, Dkt. Samweli Jasper akionesha shehena ya unga uliosagwa katika kiwanda chao na kuhifadhiwa vizuri.

’CPB inamuunga mkono Rais Samia kwa vitendo kwa kutoa huduma iliyo bora kwa Wananchi kuhakikisha wanakula vyakula vilivyopimwa na kuchakatwa kwa usahihi bila kupoteza virutubisho vilivopo katika mazao’’, alisema Dkt. Jasper.

Aidha Meneja huyo alisema Rais Samia Suluhu ametoa zaidi ya Billioni 200 katika sekta ya Kilimo hivyo CPB haina budi kufanya kazi kwa uhakika na umakini ukilenga kuwasaidia wananchi katika kupata chakula bora.

Meneja huyo alisema kuwa CPB Nyanda za Juu Kusini wamekuwa wakihudumia katika Mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Songwe, Njombe na Iringa yenyewe hivyo wananchi wa ukanda huo wamekuwa wakipata huduma ya kuuziwa bidhaa zao.

‘’Kama nilivyosema lengo la CPB ni kuinua Uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini na wa Nchi pia, hivyo tunanunua mazao kutoka kwa wakulima wa ukanda huu na kuyachakata, kusindika na kusaga alafu tunawauzia bidhaa zetu kwa bei nafuu ukilinganisha bei za sehemu nyingine’’, alisema Meneja huyo.

Aidha Dkt. alisema katika kukuza Uchumi wa Nchi CPB imekuwa ikiuza bidhaa zake nje ya nchi kama vile Rwanda, Kenya na Malawi.
Dkt. Jasper alisema bidhaa zao zipo katika kila ujazo kwani wanauza rejereja na jumla hivyo wamekuwa wakiuzia wafanyabiashara wakubwa,wakati na wadogo pamoja na wananchi wa kawaida.

‘’Tuna mtambo ambao tuliuurithi kutoka national Milling (NMC) ambao una uwezo kwa kuzalisha tani 50 hadi 55 za mahindi kwa siku ambao ukisagwa zinatoka tani 45 za unga ‘’ alisema Meneja huyo.

Hata hivyo, ili kuwafikia wananchi wote Meneja huyo alisema CPB inatarajia kuweka Mawakala wa bidhaa zao kila Mkoa ambao watakuwa wakisambaza bidhaa hizo.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Machi 20, 2023
Miradi afya ya macho kugharimu Bilioni 1.47