Meneja wa klabu ya Leicester City Craig Shakespeare amesema bado uongozi wa klabu hiyo haujapokea ofa yoyote inayomlenga kiungo mshambuliaji kutoka nchini Algeria Riyad Mahrez.

Mahrez anahushwa na taarifa za kutakiwa nchini Italia kwenye klabu ya AS Roma ambayo inaamini huduma yake huenda ikawasaidia kuanzia msimu ujao wa ligi (2017/18).

Shakespeare ameweka vyema taarifa hizo akiwa Hong Kong ambapo kikosi chake kimeweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi ya nchini England, ambao utaanza rasmi mwezi ujao.

“Riyad bado ni mchezaji wa Leicester City, na mpaka sasa hakuna ofa yoyote iliyotumwa kwetu kwa ajili yake,”  amesema Shakespeare.

“Jambo hili lipo wazi, kama kuna klabu yoyote inahitaji kumsajili Riyad inapaswa kufuata taratibu ambazo zinafahamika ulimwenguni kote, lakini taarifa za vyombo vya habari haziwezi kusaidia mpango wa kumuhamisha mchezaji huyu.”

“Binafsi ninahitaji kufanya kazi na Riyad, lakini kama itatokea mchezaji mwenyewe anataka kuondoka sitokua na kipingamizi chochote, natambua umuhimu wa maisha ya mchezo wa soka, maana leo unaweza kuwa hapa na kesho ukawa kule, ni jambo la kawada sana.”

Kikosi cha Leicester City kitashiriki michuano ya kombe la Premier League Asia, sambamba na West Bromwich Albion, Crystal Palace na Liverpool zote za nchini Engalnd.

Leicester City wataanza kampeni ya kuusaka ubingwa wa England Agosti 11 kwa kucheza na Arsenal.

Madam Flora amnyoshea kidole aliyemzushia uongo
RC Singida awapa somo watumishi wa umma, awataka wapunguze muda wa vikao