Baada ya uamuzi wa kocha wa Real Madrid kutangaza kuhusu mpango wake wa kuachana na Real Madrid nyota wa klabu hiyo, Cristiano Ronaldo amemtumia ujumbe mzito wenye hisia kali akionesha mchango wake mkubwa katika kumfanya awe mtu wa kuheshimika.

Cristiano Ronaldo maarufu kama CR7 raia wa Ureno ametumia ukurasa wake wa Instagram kumfikishia ujumbe huo mzito Zidane;

”Solo siento orgullo de haber sido tu jugador. Mister, gracias por tantisimo” akimaanisha

”Ninajivunia kuwa mchezaji wako, nakunifanya niheshimike, nakushukuru sana”.

Kupitia posti hiyo mashabiki wa mchezaji huyo walitoa maoni zaidi ya milioni sita kwenye ukurasa wake wa instagram huku wengine wakimtaka kocha huyo asiondoke timu hiyo kufuatia rekodi pekee aliyoivunja Zidane akiwa kama kocha wa timu hiyo.

Jana Mei 31, 2018 Zidane alitangaza kujiuzulu ukocha wa timu hiyo alipofanya mkutano na waandishi wa habari.

Wema apenda sifa alizomwagiwa Zari, ajiandaa kupika
Pusha T amvuruga Drake, alazimika kujieleza mtandaoni