Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo jana ameiwezesha timu yake ya taifa kuitungua timu ya taifa ya Urusi jijini Moscow katika michuano ya kombe la mabara inayoendelea nchini Urusi jijini Moscow.

Katika mchezo huo ambao uliochezwa katika dimba la Spartax jijini Moscow ulikuwa unasubiliwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa mpira wa miguu duniani kote na ambao ulikuwa ni muhimu kwa timu zote mbili kuweza kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele katika michuano hiyo.

Mchezaji bora duniani, Cristiano Ronaldo aliifungia timu yake bao pekee na la kuongoza dakika ya nane kipindi cha kwanza ambalo lilidumu mpaka dakika ya tisini ya mchezo huo hivyo kuifanya Ureno kusonga mbele katika michuano hiyo.

Hata hivyo, katika mchezo wa pili ambao ulizikutanisha timu za Mexico na New Zealanda, Mexico iliitandika New Zealand mabao 2-1 na kuiondoa katika michuano hiyo ya kombe la mabara.

Video: Kufuru ya wauza unga gerezani, Magufuli 'amtumbua' Mutalemwa Dawasa
Magazeti ya Tanzania leo Juni 22, 2017