Cristiano Ronaldo ameendelea kuwaacha njia panda mashabiki wake, kufuatia kitendo cha kutokua sehemu ya wachezaji waliopiga picha, kwa ajili ya kuonyesha jezi mpya za Real Madrid ambazo zitatumika msimu ujao wa 2018/19.

Katika picha zilizoachiwa kwenye mitandao ya kijamii zikionyesha tukio hilo, Ronaldo hajaonekana kabisa huku jezi yake pekee ikionyeshwa upande wa nyuma wenye namba 7.

Mshambulaiji huyo alianza kuwaacha solemba mashabiki wake kwa kutoa kauli tata, mara baada ya mchezo wa fainali dhidi ya Liverpool ambao ulimalizika kwa Real Madrid kuibuka na ushindi wa mabao matatu kwa moja.

Ronaldo alipohojiwa siku hiyo alisema: “Ulikua wakati mzuri nikiwa Real Madrid.”

“Nitatangaza mustakabali wangu siku chache zijazo “. Kwa sasa nitatumua wakati uliopo kushangilia ubingwa huu na wachezaji wenzangu”

Hata hivyo mshambuliaji Gareth Bale, ambaye tayari ameshaanza kuhusishwa na taarifa za kuondoka Real Madrid, ameonekana katika picha za maonyesho ya jezi mpya,jambo ambalo limeendelea kuwachanganya mashabiki wa Ronaldo.

Cristiano Ronaldo is the only first-teamer not pictured in new Real shirt (image: Real Madrid)

Ronaldo alijiunga na Real Madrid mwaka 2008 akitokea Man Utd kwa ada ya Pauni milioni 80 ambayo iliweka rekodi kwa wakati huo, na kumfanya kuwa mchezaji ghali duniani.

Mpaka sasa ameshacheza michezo 292 akiwa na The Galacticos na kufunga mabao 311.

Ronaldo ni mchezaji pekee katika kikosi cha Real Madrid aliyetwaa ubingwa wa Ulaya mara tano, mara nne akiwa na klabu hiyo ya Santiago Bernabeu na mara moja akiwa na Man Utd.

Magazeti ya Tanzania leo Mei 30, 2018
Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Iceland

Comments

comments