Nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo ameutaka uongozi wa klabu ya Real Madrid, kutofanya maamuzi ya kumuweka sokoni James Rodriguez.

James alikua tayari kwa ajili ya mchakato wa kuingizwa sokoni katika kipindi hiki, kutokana na kuhofia kiwango chake kuporomoka endapo ataendelea kubaki Estadio Stantiago Bernabeu.

Ronaldo amechukua jukumu la kuwasilisha ombi hilo, kwa rais wa Real Madrid, Florentino Perez ambaye alikua ameshapitisha baraka za kuuzwa kwa mshambuliaji huyo kutoka nchini Colombia.

Mshambuliaji huyo aliyepiga penati ya mwisho iliyoipa taji la barani Ulaya Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid mwishoni mwa mwezi uliopita katika mchezo wa hatua ya fainali uliochezwa mjini Milan nchini Italia, anaamini James bado ana uwezo mkubwa kisoka ambao unaweza kuchangia mafanikio zaidi kwa msimu wa 2016-17.

Wawili hao wamekua wakimilikiwa na wakala mmoja (Jorge Mendes), na ni mararafiki wa muda mrefu ndani na nje ya uwanja.

James amekua anahusishwa na mipango ya kutaka kusajiliwa na klabu za Manchester United na PSG, na kinachosubiriwa sasa ni amri ya kuwekwa sokoni ili kuruhusu ofa kuanza kuingia mjini Madrid.

Liverpool FC Yapanga Kumsajili Kieran Gibbs
Jamie Vardy Kufanyiwa Vipimo Vya Afya