Kwa mara ya kwanza mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amezungumzia maamuzi yaliyochukuliwa na mpinzani wake wa karibu Lionel Messi ya kutangaza kustaafu soka la kimataifa.

Ronaldo alikua anasubiriwa kwa hamu kuzungumzia maamuzi yaliyochukuliwa na Lionel Messi majuma mawili yaliyopita mara baada ya fainali za Copa Amarica za mwaka 2016 kufikia tamati nchini Marekani kwa kushuhudia Chile wakitetea ubingwa.

Mshambuliaji huyo wa klabu ya Real Madrid, amejikuta akizunguzia suala la Messi akiwa katika mkutano na waandishi wa habari nchini Ufaransa, baada ya kulizwa ni vipi alivyopokea maamuzi ya mchezaji huyo wa FC Barcelona.

Ronaldo amesema aliona taarifa hizo katika vyombo vya habari na alishutushwa na maamuzi ya Messi kutokana na kuamini kwamba haikuwa siku sahihi kwake kutoa maamuzi ya kujiondoa kwenye jukumu la kuitumikia timu yake ya taifa ya Argentina.

“Messi Amefanya maamuzi mazito ambayo ni vigumu kuyapokea, binafsi nimeshangazwa na mpaka sasa sijaamini kama kweli amejiondoa katika jukumu la kuitetea nchi yake.

“Ninaendelea kujiuliza kila kukicha kwa nini amechukua maamuzi hayo, lakini ninakosa jibu kutokana na muhusika kuwa mbali nami na ni vigumu kumuuliza.

“Imeniuma sana kuona Messi akiwa katika majonzi na kisha kuchukua uamuzi mgumu kama huo, lakini bado ninaamini ataweza kubadili mawazo na kurejea katika jukumu la kuitumikia Argentina.” Alisema Ronaldo

Ronaldo bado yupo nchini Ufaransa sambamba na wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Ureno kwa ajili ya mchezo wa hatua ya nusu fainali ya Euro 2016 utakaowakutanisha dhidi ya Wales siku ya jumatano (Kesho).

Ndoto Za James Rodriguez Kwenda PSG Zayeyuka Rasmi
Rafa Benitez: Inatosha, Hatoondoka Mwingine