Jeshi la Polisi limesema watu watatu wamefariki katika ajali iliyohusisha magari mawili na pikipiki mbili katika eneo la magunila Manispaa ya Morogoro barabara kuu ya Morogoro kuelekea Dodoma.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa Morogoro, Fortunatus Musilimu amesema tukio hilo limetokea alfajiri ya Desemba 5, 2022 baada ya gari aina ya Toyota Land Crusser lenye namba za usajili T 514 CAQ mali ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro, kugonga gari lenye namba za usajili 2032 JW 12 mali ya jeshi la Wananchi Pangawe.

Kamanda wa Polisi Mkoa Morogoro, Fortunatus Musilimu.

Amesema, “Mara baada ya gari hilo aina ya Toyota Land Crusser kugonga gari ya jeshi la Wananchi Pangawe lilipoteza muelekeo na kugonga bodaboda mbili.”

Aidha, Kamanda Musilimu amewataja waliopoteza maisha katika ajali hiyo kuwa ni madereva wa pikipiki wawili na abiria mmoja, na kusema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa gari la ofisi ya wa Mkuu wa Mkoa Morogoro, Abeid Namangaye kuyapita magari yaliyopo mbele yake bila kuchukua tahadhari.

Hata hivyo, amesema Dereva huyo kwa Sasa anashikiliwa naJeshi la Polisi kwa ajili kusibiri taratibu za kisheria na upelelezi utakapo kamilika atafikishwa mahakamani.

Hatma ya Rais Ramaphosa mikononi mwa ANC
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Decemba 6, 2022