Aliyekua kiungo wa Arsenal Mathieu Flamini, amekamilisha taratibu za kujiunga na klabu ya Crystal Palace kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32, amemalizana na Crystal Palace kama mchezaji huru, kufuatia mkataba wake na klabu ya Arsenal kufikia kikomo mwishoni mwa msimu uliopita.

Meneja Crystal Palace Alan Pardew, amethibitisha kusajiliwa kwa kiungo huyo ambaye aliwahi kuzitumikia klabu ya Marseille ya Ufaransa na AC Milan ya Italia.

“Ni kweli tumekamilisha mazungumzo na kumsajili Flamini, nina uhakika atatusaidia katika kipindi chote atakachokuwa hapa,”

“Nimekua shabiki mkubwa wa Flamini tangu akiwa Arsenal, kutokana na uwezo wake wa soka ambao amekua akiuonyesha katika ligi ya nchini England, hivyo nina imani bado ana nafasi ya kuendelea kuthibitisha hilo Selhurst Park.” Amesema Pardew.

Huruma Ya FIFA Yaibeba Sunderland, Wafanya Usajili Nje Ya Muda
Video: Wito uliotolewa na Wazee Chadema kwa Rais JPM