Chama cha Wananchi CUF kimekutana na waandishi wa habari leo Julai 21, 2016 ambapo Naibu Katibu wa chama hicho, Nassor Mazrui ameeleza msimamo wa chama hicho kuhusu mchakato wa kufungua kesi katika mahakama ya kimataifa ya ICC ili kudai haki yao.

Baada ya uchaguzi mkuu wa marudio wa Zanzibar uliofanyika March 2016, Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amekuwa na ziara za nje ya nchi kutafuta kile anachokiita haki kutokana na uchaguzi mkuu wa Zanzibar October 2015 kufutwa.

Katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amekuwa na ziara nje ya nchi tangu baada ya uchaguzi mkuu wa marudio Zanzibar March 2016 kuisha, Maalim Seif amekuwa akienda jumuiya za kimataifa kwa ajili ya kutafuta kile anachokiita haki kutokana na uchaguzi mkuu wa Zanzibar October 2015 kufutwa.

Mazrui ameeleza kuwa kama si leo au kesho Maalim Seif atakuwa the Hague nchini Uholanzi katika harakati zake za kudai haki katika uchaguzi uliofanyika october 2015.

Amesema Maalim Seif atakwenda kuelezea namna gani demokrasia ya Zanzibar na Tanzania inavyominywa kwa hivyo suala la ICC tumelipania na lazima hiyo kesi itakwenda na kila aliyedhulumiwa, aliyedhulumu atafika katika mahakama ya ICC.

 

Mashinji Awafunda Bavicha, Awapatia Mbinu za Kushinda 2020
Video: CCM iko pale pale na waliokuwa wanadhani wangeibuka hawakuibuka na hawataibuka - Kikwete