Watanzania wanaoishi nchini Uingereza ambao wanaaminika kuwa wanachama wa Chama Cha Wananchi (CUF) wameandamana hadi kwenye ofisi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo jijini London kumuomba ashinikize kutangazwa kwa matokeo ya urais wa Zanzibar.

Wanachama hao wa CUF walikuwa na bendera za chama hicho pamoja na mabango yenye jumbe mbalimbali kwa Waziri Mkuu huyo kuitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kutangaza matokeo ya Urais.

Katika hatua nyingine, baadhi ya wananchi wa Zanzibar wameonesha kuwa katika sintofahamu kufuatia uteuzi wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Khasim Majaliwa wakidai kuwa uteuzi huo kwao unashangaza kwani bado Zanzibar iko katika kiza cha kutokuwa na uongozi wa awamu mpya kutokana na tangazo la kufutwa kwa uchaguzi lililotolewa na Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha na kuchapishwa kwenye gazeti la serikali.

Lipumba amshauri Magufuli kuhusu Bajeti na hali ya Zanzibar
Dkt Shein ashauriwa kutohudhuria Bungeni leo