Chama Cha Wananchi (CUF) upande wa Prof. Lipumba wameitaka Chadema kuviongoza vyama vya upinzani kupigania haki zao wakiwa kama chama kikuu cha upinzani nchini.

Hayo yamesemwa jijini Dar es salaam na Msemaji wa Chama cha Wananchi (CUF), Abdul Kambaya alipokuwa akifanya mahojiano katika kipindi cha, East Africa BreakFast ya East Africa Radio ambapo amesema kuwa Chadema ndio chama kikuu cha upinzani hivyo kinawasubiri kiwaongezee nguvu katika kupigania haki ya kufanya mikutano ya hadhara.

Amesema kuwa kuzuia mikutano ya hadhara na maandamano ya amani kwa vyama vya upinzani ni kuvinyima haki ya msingi vyama hivyo.

“Hatuna mpango wa kujitoa katika chaguzi zozote licha ya mkanganyiko wa kisiasa uliopo kwa sasa ndani ya chama chetu”, amesema Kambaya.

Aidha, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kupitia kwa mwenyekiti wake, Freeman Mbowe walitangaza kutoshiriki kwenye chaguzi zote zitakazoendelea nchini chini ya tume ya uchaguzi iliyopo hivi sasa wakidai kuwa wanahitaji tume huru.

Hata hivyo, Mbowe aliituhumu NEC akidai inafanya kazi ya kuhakikisha chama tawala (CCM) kinashinda kwa kulazimisha matokeo hivyo hawatashiriki katika chaguzi za marudio.

Hamisa: Wanaume wengi wanapenda kurogwa
Video: Mtoto mwingine atekwa kimafia Dar, Vigogo kortini kwa kuhujumu uchumi