Chama cha Wananchi (CUF),kimelalamikia kitendo cha Chama cha Mapinduzi (CCM) kutumia mali za Serikali katika masuala ya kisiasa.

Hayo yamesemwa na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chama hicho, Mbarara Maharagande baada ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kufanya vikao vyake vya Kamati Kuu (CC) na Halmashauri Kuu (NEC) Ikulu, jijini Dar es salaam.

Maharagande amesema kuwa kama CCM wameamua kufanya vikao vyao Ikulu itakuwa inawakosea wananchi kwakuwa Ikulu sio mali ya Chama hicho.

“Kuna taarifa kuwa vikao hivyo vimepangwa kufanyika Ikulu Jijini Dar es salaam jambo ambalo kama ni kweli itakuwa ni matumizi mabaya ya rasilimali za nchi kwa maslahi ya CCM, hii haikubaliki kwani Ikulu ni ya watanzania wote” amesema Maharagande.

Hata hivyo kwa upande mwingine CUF imewataka wana CCM kutumia muda wao huo kutathmini mwelekeo wa hali ya kisiasa na kiuchumi nchini kwa maslahi mapana ya Taifa na Wananchi wake.

 

Fahamu jinsi amabvyo kula kupita kiasi husababisha vidonda tumboni
Wakazi Dar walia ukosefu wa maji