Chama cha Wananchi (CUF) kimelitupia lawama jeshi la polisi wakidai huenda Jeshi hilo limebeba ajenda ya siri ya kukidhoofisha chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mbunge wa jimbo la Mchinga ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho, Hamidu Bobali alisema kuwa wameshangazwa na kitendo cha polisi kuwazuia kufanya mkutano wao wa ndani Newala, ikiwa ni miezi michache tu baada ya kutangaza kuondoa zuio hilo.

“Tulipaswa kufanya mkutano wetu wa ndani Newala jana. Lakini katika hali ya kushangaza, Jeshi la Polisi limetuzuia kufanya mkutano huo,” alisema Bobali. “Tumeshtushwa sana na uamuzi huo kwa sababu ni siku chache tu tangu itangazwe kuondolewa zuio hilo,” aliongeza.

Bobali ambaye anaunga mkono kambi ya Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad, alihoji uamuzi wa jeshi la polisi kumruhusu Profesa Ibrahim Lipumba (Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili) kuruhusiwa kufanya mikutano katika mikoa ya kanda ya kusini.

 

 

Mashabiki wa Coastal Union wamshushia refa kipigo cha mwizi!
Video: Mtoto aliyezaliwa bila mikono ajifunza kula kwa miguu, awavuta wengi