Wakati wingu zito likitanda kuhusu uamuzi wa Chama Cha Wananchi (CUF) kususia uchaguzi wa marudio ulipangwa kufanyika Machi 20 mwaka huu, Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai ameeleza kuwa wamebaini chama hicho kinapanga kushtukiza.

Vuai Ali Vuai

Vuai Ali Vuai

Vuai ameeleza kuwa kwa mujibu wa taarifa ambazo chama chake kimezipata, CUF wanajiandaa kimyakimya na uchauzi na kwamba wanapanga kushiriki kwa kushtukiza ifikapo siku hiyo.

“Naamini CUF watashiriki uchaguzi. Nawajua sna wale ndugu zangu. Kwa taarifa tulizo nazo wanafanya maandili ya chini chini ili siku wakiibuka iwe kama shitukizo, tunawakaribisha,” Vuai anakaririwa na gazeti la Mwananchi.

Alieleza kuwa chama chake kinajiandaa na uchaguzi huo wa marudio wakijua kuwa wapinzani wao wakuu, CUF watashiriki na kwamba endapo wataamua vinginevyo itafahamika muda huo ukifika.

Hata hivyo, tamko hlio la Vuai lilipingwa vikali na Katibu Mkuu wa CUF, Zanzibar Nassor Mazrui ambaye alidai kuwa wao walishaweka wazi msimamo wao na hawabadiliki kwakuwa tayari wameshaiandikia barua rasmi Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kuhusu uamuzi wao wa kutoshiriki.

“Tumewaachia CCM wafanye uchaguzi wao, wachague serikali yao sisi tutabaki kuwa waangalizi tu na hakuna jambo lolote baya ambalo tunapanga kufanya kwa sababu biashara tulishaimaliza Oktoba 25,” alisema Mazrui.

Hivi karibuni, Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salim Jecha alieleza kuwa hakuna chama cha siasa kilichojitoa kwenye uchaguzi huo kwakuwa hakuna vyama vyote havikufuata utaratibu wa kujitoa kwa mujibu wa sheria, licha ya kukiri kupokea barua za wagombea kujitoa kwenye kinyang’anyiro hicho cha marudio.

Ndege yapotea ikiwa na abiria 21
Waziri wa JK atajwa mahakamani kesi ya Ufisadi Hifadhi ya Taifa