Chama chacha Wananchi (CUF), kimetangaza kuziba nafasi  ya Mwenyekiti wa Chama hicho ngazi ya Taifa iliyoachwa mwaka jana na Profesa Ibrahim Lipumba, pamoja na nafasi ya Makamu Mwenyekiti iliyoachwa na Juma Duni Haji.

Akiongea na waandishi wa babari jijini Dar es Salaam, Katibu Msaidizi wa CUF Tanzania Bara, Shaweji Mketo alisema kuwa nafasi hizo zitazibwa Agosti 21 mwaka huu katika kikao cha Halmashauri.

Aliongeza kuwa chama hicho kitamchagua Makamu Mwenyekiti kwakuwa nafasi hiyo iliachwa wazi baada ya Juma Duni kujiunga na Chadema ili kutimiza masharti ya kuwa mgombea mwenza wa urais wa Edward Lowassa, kabla hajarejea muda mfupi baada ya kukamilika kwa uchaguzi.

“Huu ni mwanzo wa kuhakikisha tunarudisha matumaini mapya kwa watanzania kupitia uchaguzi mkuu wa mwaka 2020,” alisema na kuongeza kuwa katika uchaguzi huo, chama hicho pia kitawachagua wajumbe wengine wanne wa Kamati Kuu.

Aliwataka wananchama wote wenye sifa za kujana nafasi hiyo kuchukua fomu ili waweze kushiriki katika kinyang’anyiro hicho.

Profesa Lipumba alijiuzulu nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho siku kadhaa baada ya Lowassa kujiunga na Chadema na kupewa nafasi ya kugombea nafasi ya urais akiungwa mkono na vyama vinavyounda Ukawa ambapo CUF ni sehemu ya muungano huo.  Alisema kuwa moyo wake ‘unamsuta’ kumuunga mkono Lowassa.

Picha: Meninah afunga ndoa tena, ambwanga mtoto wa Muhongo
Rais Magufuli atembelea kanisa la Mzee wa Upako, amuahidi haya