Chama Cha Wananchi (CUF) kimepongeza juhudi za serikali katika kukuza uchumi ikiwemo kuongezeka kwa pato la taifa.

Pongezi hizo zimetolewa Bungeni Jijini Dodoma na mbunge wa viti maalum wa chama hicho, Rukia Kassim wakati akichangia mapendekezo ya Serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2018/19.

“Naipongeza Serikali kwa hatua za kukuza uchumi hasa ukuaji wa Pato la Taifa unaotarajiwa kuwa asilimia 7.2”, amesema Rukia.

Naye Mbunge wa Urambo, Margreth Sitta ameipongeza Serikali kwa kupendekeza kusamehe kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwenye taulo za kike.

Akichangia kwenye bajeti kuu ya Serikali, Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Peter Serukamba amesema kuwa anampongeza sana Rais John Pombe Magufuli kwa kujenga miradi mikubwa miwili ya Standard Gauge na ya Umeme wa Stiegler’s Gorge.

Hata hivyo, Wabunge wanaendelea kuchangia bajeti ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2018/19 ambayo iliwasilishwa wiki iliyopita na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Phillip Mpango

Askofu mbaroni kwa utapeli wa mamilioni ya waumini
Video: Mkuchika awakingia kifua watumishi waliotumbuliwa na wakuu wa mkoa, wilaya