Chama cha Wananchi (CUF) kimempiga chini aliyekuwa Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba kuwania tena nafasi hiyo, ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu aombe kurejea kwenye nafasi yake.

Hayo yamebainika jana baada ya chama hicho kupitia kwa Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi (CUF), Shaweji Mketo baada ya kutangaza majina tisa ya wagombea wa nafasi hiyo pamoja na majina manne ya wagombea wa nafasi ya makamu Mwenyekiti, huku jina la Profesa Lipumba likiweka kando.

Majina tisa yaliyotajwa na Mketo kuwania nafasi ya Mwenyekiti ni pamoja na Abdul Omary Zowo, James Mahangi, Joseph Zhobi, Juma Nkubi, Salum Barwany, Selemani Khatibu, Twaha Taslima, Zuberi Kuchauka na Riziki Mngwali.

Aidha, Mketo aliwataka wagombea wote kuhakikisha hawatumii vishawishi vya rushwa kutafuta nafasi hiyo itakayopatikana kupitia uchaguzi utakaofanyika Agosti 21 mwaka huu.

“Yeyote atakayebainika ameshawishi kwa njia yoyote kwa kutumia rushwa jina lake litaondolewa kwenye orodha ya wagombea,” alisema Mketo.

Jina la Juma Duni Haji aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho aliyejiuzulu na kujiunga na Chadema kwa ajili ya kutekeleza masharti ya kikatiba ya kuwa mgombea mwenza wa Lowassa (Chadema), ameomba tena nafasi hiyo baada ya kurejea.

Nafasi ya uenyekiti wa CUF iliachwa wazi na Profesa Lipumba mwaka jana, siku chache kabla ya kuanza kampeni za uchaguzi mkuu akipinga kitendo cha chama hicho kupitia Ukawa kumsimamisha Edward Lowassa (Chadema) kugombea urais.

Ni Usain Bolt Tena, Atwaa Medali Ya Tatu Mfululizo
Ndugai: Wapinzani kutoka nje ya Bunge ni Haki yao, lakini…