Chama cha Wananchi (CUF) kimemtaka Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe kuacha kumtolea lugha za kejeli na maudhi, Prof. Ibrahim Lipumba.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano ya Umma, Abdul Kambaya ambapo amesema kuwa kauli zinazotolewa na Mbowe kuhusu CUF na mwenyekiti wake zinaonyesha kuwa chama hicho kimekosa mwelekeo.

Amesema kuwa kutokana na kauli hizo inaonekana Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimeamua kuanzisha mashambulizi yasiyokuwa na tija dhidi ya CUF, hivyo amewataka wananchi kutowasikiliza.

Aidha, ameongeza kuwa Mbowe anatakiwa atambue sababu za Prof. Lipumba na Dkt. Willbrod Silaa kutoshiriki katika kampeni za uchaguzi mkuu wa urais uliopita kulitokana na mgombea wa Ukawa kukosa sifa za uadilifu na kukabiliwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi.

Hata hivyo, katika siku chache zilizopita, akiwa katika uzinduzi wa kampeni za udiwani Mtwara Mjini, Mbowe alisema kuwa hamheshimu Prof. Lipumba na kumuita kuwa ni Profesa wa ajabu, pia kuhoji uhalali wa elimu ya Prof. Lipumba alikoipata.

Ruge afunguka kuhusu ndoa ya Zamaradi, ‘hatubusu na kusimulia’
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Novemba 14, 2017