Rais wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Ahamd Ahmad amesema kuwa ameridhishwa na maandalizi ya michuano ya Afrika ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (AFCON).

Ameyasema hayo wakati akizungumza na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika makazi ya Waziri Mkuu, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Mashindano ya mpira wa miguu kwa Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 AFCON yanayotarajiwa kufanyika mwaka 2019 nchini Tanzania.

Aidha, Ahmad ameihakikishia Serikali kwamba hakuna mabadiliyo yoyote ya ratiba yatakayofanyika kuhusu wenyeji wa mashindano na kwamba CAF itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kufanikisha michuano hiyo.

Rais wa CAF yupo nchini kwa ajili ya kuongoza mkutano maalum wa mabadiliko ya katiba ya Baraza la Vyama vya Soka katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

 

Video: Dkt. Mpango akomaa na makontena ya Makonda
NEC yawapiga msasa wasimamizi wa uchaguzi