Mkurugenzi wa jiji la Tanga Daudi Mayeji ametangaza kuwavua udiwani madiwani watatu wa CUF mkoani humo baada ya kupokea barua ya kuvuliwa kwao uanachama na naibu katibu mkuu wa chama hicho bara Magdalena Sakaya.

Madiwani hao ni Rashid Jumbe wa kata ya Mwanzange, ambaye ndiye Mwenyekiti wa CUF wilaya ya Tanga, Fatma Hamza Mbunge viti maalum, na Halima Mbwana ambaye naye ni mbunge wa viti maalum.

Katika barua iliyoandikwa julai 7, imeeleza kuwa wanachama hao walivuliwa uanachama kwa sababu tatu, ya kwanza ikiwa ni kuvuruga chama kwa makusudi, kukaidi wito wa baraza la uongozi na kosa la tatu ni kuwavuruga wanachama CUF.

Sakaya alipeleka barua hiyo ya kuwavua uanachama madiwani hao Ijumaa wiki iliyopita kwa kile alichosema walikataa kuweka mgombea katika kata ambazo zilibaki wazi baada ya madiwani wa CUF kuhamia CCM.

”Wale madiwani akiwamo mwenyekiti wa CUF wilaya ya Tanga, walikataa kuweka mgombea maeneo ambapo madiwani wetu walihamia CCM, wakaanza malumbano wakisema wamepewa maagizo tuweke wagombea wa Chadema.

Ameongezea ”hatuwezi kuvunja katiba bila sababu za msingi chama kinaongozwa kwa katiba. Inashangaza mtu kulazimisha awekwe wa chama kingine” amesema Sakaya.

 

Video: Waziri Jafo atangaza ajira 6,180 watumishi afya
Dereva wa Trump amfungulia shitaka la madai

Comments

comments