Polisi nchini India wanamtafuta Daktari feki kwa kusababisha zaidi ya watu 21 kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Ambapo taarifa iliyotolewa na Afisa wa afya wa India inasema kuwa daktari huyo feki amekuwa akiwatibu wanakijiji wenye magonjwa ya kuharisha, vifua na mafua kwa kutumia sindano moja.

Daktari huyo anajulikana kwa jina la Rajendra Yadav ambaye ametoroka kijijini hapo, Bangarmau kufuatiwa na tuhuma hizo zinazomkabili.

Wanakijiji wamesema ni mara chache sana walikuwa wakimuona daktari huyo kubadili sindano. Kitu ambacho Afisa anasema inawezekana kuwa sababu ya maambukizi hayo ya VVU

Kutokana na uchache na ugumu wa kupatikanaji wa Madaktari, Watu wa India wamekuwa wakitafuta Madaktari feki kwa matibabu ya bei ndogo.

 

Nassari afikishwa mahakamani
Aliyemuua Bob Marley ajitokeza, adai kutekeleza mpango wa Marekani kuwaua...

Comments

comments