kati ya matukio ambayo yamefunga mwaka 2016,  huwezi kuacha kulitaja hili la mkulima Augustino Mtitu aliyechomwa mkuki mdomoni na ukatokea shingoni kwa kile kilichoelezwa mgogoro wa wafugaji na wakulima huko kijiji cha Dodoma Isanga kata ya Manzese wilaya ya Kilosa Morogoro.

Dk. Francis ambaye ni daktari bingwa wa upasuaji katika hospitali ya mkoa wa Morogoro, Dk. Francis ndiye aliyempokea mgonjwa na akamfanyia upasuaji wa kumtoa mkuki….

‘Wengine wanafikiri mkuki uliingia mdomoni kabisa lakini ukweli ni kuwa mkuki ulikita katikati ya pua na mdomo, kwa bahati nzuri ulipita ukakwepa hata mifupa ingawaje taya la juu liliguswa kidogo tunaweza kusema huyu ni Mungu tu aliyemuokoa wala si daktari kwa sababu kuna sehemu zingeguswa hata Hospitali asingefika’ 

Mambo 10 ya kufanya 2017 iwe ya mafanikio
Uvumilivu ni silaha katika kusaka mafanikio