Hospitali ya Taifa Muhimbili, (MNH) imethibitisha kuwa Daktari bingwa na mshauri wa magonjwa ya watoto wachanga Augustine Massawe amefariki dunia leo agosti 13, 2021 katika hospitali hiyo alipokuwa akipatiwa matibabu.

Taarifa hiyo imethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano kwa umma Muhimbili, Aminiel Aligaesha amesema kuwa Dokta Massawe amefariki saa mbili na nusu asubuhi leo.

Aidha amesema kuwa Dkt. Massawe ni daktari maarufu ambaye amekuwe akitibu Watoto tangu mwanzoni mwa miaka ya 1980 na alipata umaarufu mkubwa katika jiji la Dar es Salaam kutokana na huduma ambayo alikuwa akiitoa.

Kutokana na kujituma kwake, licha ya kustaafu miaka 10 iliyopita Muhimbili ilimuomba aendelee kutoa huduma na hadi anafariki alikuwa bado akihudumia watoto hospitalini hapo na akiendelea kufundisha wanafunzi wa udaktari katika Chuo Kikuu kishiriki cha Afya na Sayansi Muhimbili (Muhas).

“Baba amefariki asubuhi ya leo alikuwa anaumwa na alilazwa Muhimbili kwa zaidi ya wiki na leo saa tatu asubuhi Mungu akamchukua,” amesema mtoto mkubwa wa Massawe  Dkt. Furaha ambaye ni daktari wa magonjwa ya kina mama na uzazi.

Rais Samia azungumza na Eng Ahmed El Sewedy mwekezaji kutoka Misri
Ulega awahasa wakulima na wafugaji