Daktari wa klabu ya Chelsea, Eva Carneiro ameripotiwa kupewa adhabu na mkuu wa benchi wa klabu hiyo, Jose Mourionho kwa kutakiwa kutokukaa kwenye benchi wakati wa michezo itakayowahusu kwa sasa.

Mvurugano uliotokea baina ya daktari huyo na Jose Mourinho mwishoni nwa juma lililopita wakati wa mchezo wa ufunguzi wa ligi ya nchini England dhidi ya Swansea City, umetajwa kuwa chanzo cha kutolewa kwa adhabu dhidi ya Eva Carneiro.

Mourinho, alimbwatukia Eva Carneiro na kumuita mzembe, baada ya kuonekana kuchukua muda mrefu kutoa huduma ya kwanza kwa kiungo mshambuliaji Eden Hazard, kitendo kilichochukuliwa kama kuchelewesha muda wa kusaka bao la ushindi kwa wenyeji Chelsea.

Mourinho anadai mchezaji wake Eden Hazard hakuhitaji matibabu kwa sababu alikuwa amechoka.

Fununu za adhabu kwa daktari huyo, ziliibuliwa na gazeti la Daily Telegraph ambapo inadaiwa Eva Carneiro hatoruhusiwa kukaa kwenye benchi, kufika mazoezini pamoja na kuambataka na timu kwenye hoteli yoyote watakayoweka kambi.

Hata hivyo taarifa hizo zimesisitiza kwamba Eva Carneiro ataendelea kuwa mkuu wa kitengo cha utabibu cha Chelsea kama mkataba wake unavyoelekeza.

AY: Wasanii Wa Bongo Tukimbie
Mbowe Azungumzia Afya Yake Akiwa Muhimbili