Daktari wa timu ya taifa ya Argentina amesema mshambuliaji wa klabu ya Manchester City Sergio Aguero atakuwa nje ya uwanja kwa takribani wiki sita baada ya kupata ajali ya gari na kuvunjika mbavu.

Taarifa za awali kutoka katika klabu ya Man City zilidai kuwa Aguero angekaa nje ya uwanja kwa wiki mbili mpaka nne lakini Donato Villani ambaye ni daktari wa timu ya taifa ya Argentina amesema mshambuliaji huyo atakuwa nje kwa muda mrefu zaidi.

”Anajiskia vibaya sana kwasababu alitaka kucheza michezo yakimataifa lakini tukio hili la ajali limemfanya akose michezo yote miwili katika timu ya taifa”, alisema Donato Villani.

 Aguero, ambaye amefunga mabao saba katika michezo nane msimu huu, yuko nyuma kwa bao moja kufikia rekodi ya mabao 177 katika klabu ya Man City iliyowekwa na Eric Brook mwaka 1939.

Mshambuliaji huyo alipata ajali wiki iliyopita baada ya taxi aliyokuwa akisafiria kuacha njia na kupata ajali huko Amsterdam Huolanzi.

Yanga kumkosa Ngoma kwa wiki moja
Kortini kwa kusambaza taarifa za uongo mazungumzo ya Serikali na Acacia