Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) imewataka Wamiliki wote wa daladala wanaotumia kituo cha Gerezani jijini Dar es salaam kuondoa gari zao ndani ya kituo hicho ili kupisha ujenzi wa miundombinu ya Mabasi yaendayo Kasi.

Taarifa iliyotolewa rasmi na DART imesema kuwa ujenzi huo utahusisha barabara ya Kilwa kuanzia katikati ya Jiji la Dar es salaam hadi Mbagala Rangi Tatu na barabara ya Kawawa kuanzia Magomeni, Barabara ya Chang’ombe, Mgulani hadi makutano ya barabara ya Kilwa na eneo la Mgulani JKT.

Aidha katika hatua nyingine, Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini, (SUMATRA) imetoa utaratibu utakaotumika kwa safari za daladala zilizokuwa zinatumia kituo hicho kwa safari.

Bomu aliloficha bwana harusi lamuua yeye na mpambe wake
Video: Fahamu Ini linavyofanya kazi mwilini na umuhimu wake