Beki kutoka nchini Uholanzi, Daley Blind amevishukia vyombo vya habari vya England kwa kusema havikumtendea haki meneja Louis van Gaal ambaye jana alionyeshwa mkono wa kwaheri huko Old Trafford.

Blind, alisajiliwa na Van Gaal mwaka 2014 akitokea nchini kwao Uholanzi alipokua akiitumikia klabu ya Ajax Amsterdam.

Beki huyo mwenye umri wa miaka 26, amesema kwa kiasi kikubwa vyombo vya habari vya England vimechangia kwa Van Gaal kundolewa na uongozi wa Man Utd, kutokanana taarifa za mlengwa wa kushoto ambazo ziliandikwa na kuzungumzwa dhidi yake.

Amesema meneja huyo ambaye aliiwezesha Uholanzi kumaliza katika nafasi ya tatu wakati wa fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 kule nchini Brazil, hakupewa nafasi ya kuzungumzwa vizuri kila mara katika vyombo vya habari, na matokeo yake jamii ilimuona hafai kuendelea na kazi yake mjini Manchester.

“Meneja wa klabu kubwa hapa England, siku zote anakua katika wakati mgumu, hasa linapojitokeza suala la vyombo vya habari ambavyo vimekua vikiandika habari mbaya kwa asilimia kubwa.

“Naamini Louis van Gaal amefanikiwa kwa kiasi kikubwa tangu alipoanza kazi Old Trafford, hivyo alistahili kuonyeshwa heshima ya aina yake, lakini imekua tofauti.

“Naamini ni kundi dogo la watu ambalo lilipanga kumng’oa Van Gaal, ambalo ni miongoni mwa waandishi wa habari na wamefanikiwa.” Alisema Blind

Van Gaal, alitangazwa kutimuwa kazi jana mchana, ikiwa ni siku mbili baada ya kufanikisha mpango wa kuipatia ubingwa wa kombe la FA, Man Utd ambayo ilikua na ukame wa mataji tangu alipoondoka Sir Alex Ferguson.

Madiwani wamtetea Kitwanga, Watoa tamko zito
Everton Wajipanga Kumnusuru Joe Hart