Mzozo ulioibuka baada ya kiwanda cha Saruji kilichopo Mkoani Mtwara kinachomilikiwa na bilionea namba moja Afrika, Aliko Dangote, kusitisha uzalishaji, kwa kile kilichoeleza kuwa ni hitilafu za kiufundi, sasa umevuka mipaka ya nchi .
Aidha, hatua hiyo ya Kiwanda cha Dangote kusitisha uzalishaji kinachokadiriwa kuajri wafanyakazi 10,ooo imeibu sintofahamu ambayo kwa takribani wiki moja sasa.
Jarida Maarufu Duniani la Forbides linaliofuatili nyendo za kibiashara za watu wenye utajiri mkubwa Duniani limedai kuwa uamuzi huo wa Menejimenti ya Dangote kusitisha uzalishaji umetokana na kuongezeka kwa gharama kubwa za uendeshaji kiwanda hicho.
Sababu nyingine iliyotajwa na Jarida hilo kupitia tovuti yake ni kile kinachadaiwa kutozingatiwa kwa makubaliano ya mkataba, ambao Serikali haijatimiza wa kuiondolea kampuni hiyo ushuru wa forodha katika mafuta ya diezeli ambayo imekuwa ikiyaingiza nchini kwaajiri ya kuendesha mitambo yake.
Kwa Mujibu wa Forbeds kiwanda hicho kiliomba kwa Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania TPDC kusaidia upatikanaji wa gesi asilia kwa bei nafuu lakini maombi hayo yaligonga mwamba.