Beki wa kulia wa Barcelona Dani Alves amesema kwamba Cristiano Ronaldo lazima atarajie kupata lawama nyingi baada Real Madrid kupata kipigo kitakatifu kutoka kwa Barcelona.

Ushindi wa Barca wa mabao 4-0 dhidi ya Real Madrid katika dimba la Santiago Bernabeu Jumapili wiki iliyopita, umeongeza presha kubwa kwa kocha wa Rafael Benitez, vilevile rais Florentino Perez na staa wa timu hiyo Ronaldo.

Lakini Dani Alves amekataa kutoa pole kwa mahasimu wao, akisema kuwa ukosoaji huo unatokana na Madrid kujaa wachezaji wenye majina makubwa kama Cristiano Ronaldo.

“Bado atabaki kuwa Cristiano tu-mchezaji wa kiwango cha juu. Pengine hilo ndiyo tatizo”, aliwaambia wanahabari.

“Ni kivipi naweza kusema hili? ni mchezaji mwenye hamu ya mchezo muda wote, muda wote anapenda kuwa mhusika mkuu. Kama unataka kuwa kama hivyo, basi kubali yote, maana mnaposhinda watu wanakuongelea na kukufanya kama kioo chao, lakini ukipoteza lazima pia uwajibike kwa hilo”.

“Kama timu haifanyi vizuri, basi wewe ndiyo wa kulaumiwa”.

“Lakini tunakiwa kujihofia wenyewe na si Cristiano. Kusema ukweli, mimi sijali nini anafanya Cristiano”.

Watu wengi walikuwa wakimnyooshea kidole Perez kwa kumteua Benitez kuwa kocha wa Madrid lakini mashabiki wa Madrid walimzomea Benitez wakidai uwezo wake ni mdogo kuifundiha klabu hiyo.

Thomas Muller Ajiweka Kwenye Kumbukumbu Ulaya
Mtola Wa Simba Atimkia Geita Kwa Magufuli